Muhitimu wa chuo nchini Tunisia ambaye aliamua kujitoa mhanga kwa kujichoma moto akipinga kukosekana ajira nchi nzima katika taifa hilo la Afrika Kaskazini amefariki dunia.Mohamed Bouazizi (26) alifariki dunia juzi jioni hospitalini nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis. Kabla ya kifo chake jamaa huyo alikuwa akiuza matunda na mboga mboga kinyume cha sheria katika mji wa sidi Bouzid baada ya kukosa ajira. Mwezi uliopita aliamua kujimwagia mafuta ya petrol na kujitia kiberiti baada ya polisi kuharibu bidhaa zake kutokana na kutokuwa na kibali maalum.