Wanafunzi watatu wa kidato cha nne katika shule ya wasichana ya John Baptist iliyoko Boko jijini Dar es Salaam wamefariki dunia papo hapo baada ya kuzama katika maji wakati walipokuwa wakiogelea katika ufukwe wa bahari na wengine watatu kuzimia.
Akizungumza jana Kamanda wa Mkoa wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10:00 jioni wakati wanafunzi wa shule hiyo walipopelekwa kwenye ufukwe wa bahari wa eneo la Ununio kwa ajili ya mazoezi ya viungo.
Alisema wanafunzi hao walipelekwa katika zahanati ya Ununio kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.