Aliyekuwa msaidizi wa Rais Jacob Zuma, Schabir Shaik, alikamatwa alipokuwa katika kifungo cha nje kwa ajili ya afya yake.Bw Shaik, ambaye aliwahi kuwa mshauri wa masuala ya fedha, alishikwa akiwa nyumbani kwake huko Durban baada ya kumshambulia Muislamu mwenzake nje ya msikiti Ijumaa tarehe 11.(Pichani bwana Shaik akitoa maelezo kwa vyombo vya habari).


Tukio hili ni baada ya shutuma kutoka kwa mwandishi wa habari mmoja aliyedai kuwa alizabwa kibao na mfanyabiashara huyo wakiwa kwenye uwanja wa gofu.
Shaik anashtakiwa kwa ubadhirifu ulioathiri kazi yake ya siasa.
Mwaka wa 2005 Shaik alihukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa mashtaka ya ufisadi na udanganyifu, pamoja na kudai hongo kutoka kwa kampuni ya silaha na kuficha stakabadhi za deni za Zuma zilizokuwa bado zinadaiwa.