Majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi yamezidi kufanya mashambulio ya anga katika eneo la bandari ya mafuta linaloshikiliwa na waasi Ras Lanuf, katika mapigano mapya.
Walioshuhudia walisema ndege za kivita zimeangusha makombora
katika maeneo waishio watu na karibu na maeneo waishio waasi.
Hapakuwa na taarifa zozote za mauaji.
Wakati huo huo, msemaji wa waasi alisema mwakilishi wa Kanali Gaddafi alipendekeza kufanya mazungumzo atakapoondoka.
Msemaji huyo alisema, waasi hao walikataa pendekezo hilo.