Ilikuwa kazi kwelikweli pale Binti yangu alipoonekana na rafiki zake shuleni,yani ilikuwa Full shangwe,mpaka naondoka shuleni hapo walikuwa bado wanakumbatiana utasema hawakuonana miaka miingi kumbe kawiki kamoja ka mapumziko.tofauti za shule za huku na kule nilikozaliwa mimi huwa hawavai Uniform(sare za shule) ni nguo za nyumbani  mwendo mdundo tu.