Malkia wa pop,Lady Madonna ambaye ameelekeza akili yake kwenye nchi ya Malawi amesema kuwa analipa suala la elimu kipaumbele sana nchini humo kwa kuwa wengi wa watoto wadogo hawaendi shule.Akisisitiza msingi wa elimu kuwa ndio kila kitu katika maisha asilimia 67 ya wasichana hawaendi shuleni" kitu ambacho sikubaliani nacho kabisa kwa watoto wa kike kukosa elimu"alisema.Madonna ambaye alimchukua binti mmoja mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 6 na kumfanya kama mwanawe wa kufikia.Madonna amesema kuwa atagharamia kiasi cha dola milioni 15 kujenga shule kubwa itakachochukua wasichana wasiopungua 400 ili kuendeleza watoto wa kike kielimu.