Ni marufuku kwa yeyote kuvuta sigara kwenye migahawa nchini Belgium.Imetangazwa rasmi na hatua hii itaanza kutumika tarehe 30 mwezi june mwaka huu.Hali hii ya kupiga marufuku ilishatangazwa hapo awali ila ufuatiliaji wa wavutaji ulikuwa si makini,sheria hii mpya ambayo itawachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaokiuka amri hii.kwa wavutaji wote wa sigara wanatakiwa kuvuta sigara sehemu maalumu ambazo wanazijua na kuwekewa matangazo.