Anajulikana kama Ticha mwenye jina halisi la Juma Mohammed,ni mtanzania mwenye masikani yake nchini Holland.Ticha ni msanii mahiri wa siku nyingi nchini Holland,amekuwa katika game kwa muda mrefu hivi sasa ila kazi zake nyingi amekuwa akiziuza hapahapa Ulaya.Kijana Juma ni mjasilimali wa ukweli na mchungu hasa wa maisha.Amefanikiwa kufanya kazi na wanamuziki mbalimbali wa kimataifa,hivi sasa amefyatua single moja kali sana ambayo inatamba katika redio kubwa nchini Holland.
Juma Mohammed hivi sasa anamiliki studio yake mwenyewe ya muziki inayojulikana kama APACHE RECORDS iliyopo katika kitongoji kidogo kiitwacho HELMOND nchini Holland.Ticha ameahidi kufanya vyema zaidi na zaidi kwani amekuwa chini ya mafunzo makali kwa kuwa na Producer wake Walid.Maganga One Blog imefanya mahojiano moja kwa moja na Msanii huyo mkali wa ku'rap Juma Mohammed a.k.a Ticha na mahojiano hayo yatawekwa hewani kwenye ukurasa wa Blog jumamosi hii.moja ya nyimbo kali inayotamba hivi sasa ya Juma Mohammed(Ticha) ni hii hapa,gonga link hii  http://www.538juize.nl/uploads/dyd/ey-baby/ au www.538juize.nl