NA GLADINES MUSHI -ARUSHA
Mabomu yarindima Arusha kuanzia saa 11Asubuhi baada ya wanachama na wapenzi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kufanya mkesha ambapo waliwasha moto wa matairi na wengine kuanza kuyashambulia magari kulikopelekea polisi kuvurumisha mabomu ya machozi na baadhi ya viongozi wa chama hicho kushikiliwa na polisi akiwemo katibu mkuu wa chama hicho Wilbroad Slaa .

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Akili Mpwapwa alisema kuwa walifanyakazi ya ziada kuwatawanya wafuasi hao walikuwa wamedhamiria kuvunja magari vioo na kuharibu mali za raia sanjari na uvunjifu wa amani kwa raia waliokuwa wanapita kwenye maeneo ya karibu na maeneo ya uwanja huo.
Ndipo jeshi la polisi likaanza kuvurumisha mabomu yasio na idadi kuwatawanya na hatimaye kufanikiwa kumtia mbaroni katibu mkuu wa chama hicho pamoja na mbunge wa singida kaskazini Tundu Lissu huku mwenyekiti wa chama hicho akiingia mitini kusikojulikana.
Gumzo lililopo katika jiji hili ni kuhusu mkutano wa jana na mkesha uliotangazwa na mwenyekiti wa chadema kuwaamuru kufanya mkesha huo wakishinikiza mbunge wa Arusha mjini kuachiwa bila ya masharti yeyote na mahakama ya hakimu mkazi wa Arusha.
Huku baadhi ya wakazi wa Arusha wakiondolewa hofu kuendelea na shughuli zao kama kawaida hali ya hofu miongoni imetanda kwenye viunga vya jiji la Arusha na polisi wametanda kila kona kuhakikisha usalama wa mali za raia unakuwepo.
Sababu kubwa ya songombingo hilo ni baada ya mahakama ya hakimu mkazi kukataa kutoa dhamana kwa mbunge kuwa hajakidhi masharti ya mahakama hali iliyopelekea mwenyekiti wa chama hicho kuwataka wafuasi wa chama hicho kukutana kwenye viwanja vya NMC kwa kupeana taarifa zayaliyojiri mahakamani.
Hali ndani ya viwanja vya mahakama ilikuwa ni ya vurugu na kelele hadi mwenyekiti wa chama hicho alipowaamuru kukutana viwanja vya NMC na ndipo kukawa na hali shwari na shughuli za mahakama kuendelea kama kawaida kulikohanikizwa na kelele za people power.