Mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza kwa takribani masaa manne bila kupumzika imeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za usafirishaji kwa njia ya anga kutokana na maji mengi kujaa katika uwanja wa ndege wa jijini humo.
Hakuna Ndege yeyote iliyoondoka wala kutua leo jijini Mwanza maana hali ilikuwa ni mbaya sana.
Wafanyakazi mbalimbali wa kiwanja cha Ndege cha Jijini Mwanza wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda katika eneo hilo.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza wakiendelea kufanya taratibu ya kuweka vitu sawa katika chumba cha kupita abiria wanaosafiri.