PETE ya uchumba inayoning’inia kwenye kidole cha super model wa Kibongo, Jacqueline Patric aliyovishwa hivi karibuni ina thamani ya shilingi milioni tano na ushee, Ijumaa Wikienda limenusa.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa staa huyo, pete hiyo aliyovishwa na mchumba’ke anayetarajia kumuoa ‘soon’, ina mchanganyiko wa madini ya Tanzanite, Dhahabu na Almasi.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimwendea hewani Jack ili kujua ukweli ambapo alikiri na kusema:
“Ni kweli nimevishwa pete yenye thamani hiyo, lakini nilikuwa sikutaka kuweka wazi kwa sababu siyo lazima kila mtu ajue.”