Hapa ni Den Haag Centraal,kituo kikubwa cha usafirishaji wa Trein,mabasi na tram..kwa wakazi wa Den haag wakifika hapa usafiri wao wa jiji huwa rahisi kwa kuwa wanaunganishwa na kila aina ya usafiri.
Hapa ni mji mwingine wa Rotterdam nchini Holland,jiji la Rotterdam ni zuri na kubwa kwa utalii,watalii wengi wamekuwa wakivutiwa na mji huu kutokana na kutokuwa bize kama Amsterdam.
Majengo ya kisasa yaliyojengwa kiufundi zaidi yakivutia taswira ya mpita njia hata mtazamaji wa blog.
Barabara na mji wa Rotterdam ni msafi sana,angalia huo mzungo wa barabara jinsi ulivyomsafi na unavyovutia kwa wapita njia.majengo yaliyojengwa kwa mpangilio mzuri pembezoni mwa barabara,mfumo mzuri wa miundo mbinu unasaidia muonekano mzuri wa mji.


 Usafiri wa tram ni moja ya usafiri mwepesi sana kwa nchi za ulaya,hapa mmoja kati ya abiria akisubiri tram yake ili apelekwe anakokwenda.kwa mbali unaweza kuona tram nyingine ikiwa inakuja na huku baadhi ya watu wakivuka barabara na kuelekea makwao.Hapa ni Rotterdam nchini Holland.
 Utunzanji wa mazingira ni jukumu la kila raia kwa wenzetu,kwa macho yako unaweza kuona jinsi gani watu wanavyotunza mazingira yao,maana kwa sisi wafrika tumeshazoea mazoea ya kuchafua mazingira kwa kuchora kuta zetu na kutupa takataka hovyo.tujifunze kuwa na jukumu la kila mmoja kutunza mazingira yetu.
Ukiwa mtazamaji mzuri wa Movies,msikilizaji mzuri wa muziki na pia kama unapendelea katuni,pichani ni kundi maarufu duniani Orchestra ambalo huwa ni wataalam sana wa kuingiza sauti nzuri na nyororo kwenye movie nyingi sana,na pia huwa wanatengeneza katuni na mengi mazuri juu ya burudani,pichani wakiwa wanawapa burudani wananchi ndani ya jiji la Den Haag hapo jana.

Wananchi waliofurika kwa wingi kushuhudia burudani toka kwa kundi la Orchestra wakifutilia mtiririko mzuri wa burudani toka kwenye kundi hilo hapo jana.Picha zote na maelezo toka kwa Hija wa Maganga One Blog Den Haag Holland.