Hapa kuna masharifu,mawalii, walimu,pamoja na wanafunzi wakisheherekea mwaka mpya wa Kiislamu.
Wamependeza sana kwa kuvaa sare ya kijani na nyekundu wakiwa ni wanafunzi wa madrasa mbalimbali waliojumuika pamoja na kuwa kitu kimoja.
 Furaha ilioje kwa watoto kuonyesha ishara ya upendo wa dini yao na kujali siku miezi pamoja na mwaka wa Kiislamu.
Masha-Allah watoto wa taifa la kesho wakiwa wapo katika msimamo wao pamoja na wazee wao hivyo ndivyo ilivyokuwa siku hiyo adhimu ya kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu.