Tumezoea kwamba red Carpet mpaka akanyage kiongozi wa juu,tofauti na nchi za wenzetu huku Ulaya kwamba kila mmoja mwenye sehemu yake ya biashara anaweza kuweka red carpet kwa heshima ya wateja wake wanaotembelea maeneo ya biashara hiyo.Hapa ni moja ya sehemu za mji wa Den Haag nchini Holland pakiwa pamependeza kwa marembo ya matayarisho ya Christmass na New Year.

Tukiwa bado mitaa ya jiji la Den Haag unaweza kuona wenzetu jinsi gani walivyojiandaa na sikukuu hiyo ya Christmass.
Ukibahatika kupita madukani unaweza kuona jinsi gani palivyopambwa kwa kila aina ya mapambo na kuleta mvuto ambao unavutia kutazama.
Sio tu mitaani na madukani,wenzetu kwa kuwafundisha hata watoto wao nini maana ya sikukuu na jinsi ya kupamba pindi watakapokuwa wakubwa,wamewawekea mapambo mazuri shuleni.hapa ni moja ya shule ya chekechea jijini Den Haag.(picha zote na Hija wa Maganga One -Holland).