Wapiga picha wakiwa kazini wakati wa ziara ya Rais Jakaya Kikwete alipotembelea maonyesho ya miaka 50 ya uhuru jana viwanja vya Sabasaba. Juu ni Robert Okanda wa Daily News akilenga Kamera yake ili kupata taswira nzuri ya Rais huku akiwa amenga'ata midomo na chini ni Richard Mwaikkenda wa Jambo Leo akiperuzi Kamera yake kuona kama amepata taswira nzuri kwa ajili ya gazeti lake analolifanyia kazi (PICHA NA IKULU)