Uvumi ulioenea katika jamii kuwa Msanii wa Maigizo na vichekesho Joseph Shamba almaarufu Vengu amefariki dunia si wa kweli na umekanushwa vikali.

Kwa mujibu wa mmoja wa wasanii wa kundi hilo la Ze Original Komedi, ambaye hata hivyo hakupenda kutaja jina lake kwani si msemaji halali wa Kundi hilo na kunitaka Niwasiliane na Sekion David juu ya taarifa kamili ya msanii huyo.

“Achaneni na uzushi huo..mshikaji bado yupo hai na Mungu anazidi mpigania na hali yake hivi sasa inaendelea vyema,” alisema msanii huyo.

Aidha Seki alipotafutwa alidai kuwa Vengu ni mzima na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa.
Seki pia alibainisha kuwa hivi sasa suala la kuzungumzia afya ya Vengu kiundani lipo kwa wanafamilia isipokuwa wao wanajua Vengu bado mzima.