Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia mkutano wa 14 wa kimataifa wa Mazingira unaojumisha Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika, mkutano huo wa siku tano unafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha na unazungumzia mkakati wa maendeleo endelevu ya uchumi wa kijani pamoja na hali ya Mazingira katika Bara la Afrika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kompyuta kuashiria kuzindua rasmi mkutano wa 14 wa kimataifa wa mawaziri wa Mazingira kutoka nchi za Afrika unaofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha jana jioni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa 14 wa Mazingira unaojumuisha Mawaziri wa Mazingira kutoka Barani Afrika. Mkutano huo ulianza jana katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa (AICC) jijini Arusha na unatarajiwa kudumu kwa siku tano.