Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akitoa mada kuhusu Taratibu za kufuata katika kuzalisha, kuingiza na kusajili dawa nchini kabla ya kuingia sokoni kwa wajumbe wa kituo cha Uwekezaji kutoka China na wawekezaji wa Sekta ya Dawa Nchini Tanzania. Mkutano huo ujulikanao Kama "Ushirikiano na Biashara za Dawa na vifaa tiba kwa nchi za Afrika Mashariki na China" umefanyika Leo katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo. 
Mada ikiendelea kutolewa kwa washiriki wa mkutano huo.