Jeshi la wapiganaji wa Syria linasema kuwa limeondoa makao makuu yake kutoka Uturuki na kuyahamishia Syria.Kamanda wa wapiganaji alisema lengo ni kuunganisha makundi yanayopigana kumpindua Rais Bashar al-Assad.
Alisema makao makuu sasa yako katika eneo alilosema eneo la Syria lilokombolewa.
Jeshi hilo la wapiganaji limelaumiwa siku za nyuma kwa kuongoza kutoka Uturuki, na kutoweza kudhibiti wapiganaji walioko ndani ya Syria.
Inafikiriwa kuwa linategemea Uturuki kwa zana nyingi.