Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala (kulia) akiwakaribisha ofisini kwake wageni kutoka Malawi na Sierra Leone ambao wako nchini Tanzania kujifunza masuala mbalimbali ya utendaji kazi yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala (upande wa kulia katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Geoigiana Kamara (kulia) kuhusu utendaji kazi wa Ofisi ya Rasilimali watu ya Sierra Leone.
Afisa Tawala Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Chele Ndaki akitoa maelezo ya namna Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa wageni kutoka Malawi na Sierra Leone ambao wako nchini Tanzania kujifunza masuala mbalimbali ya utendaji kazi yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Naibu Katibu wa Idara ya Zimamoto na Uokaji, Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Donarld Ndagula (kushoto) akimsikiliza Bw. Abel Mwamlima kutoka Idara ya Utumishi wa Umma,Sera, Utafiti na Maendeleo kutoka nchini Malawi (aliyeshika kalamu) wakati wa kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu katika shughuli za utumishi wa Umma kati ya Tanzania,Malawi na Searra Leone.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.