Wapelestina wapatao sita wameuawa katika mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Israel katika eneo la Gaza katika siku inayohesabika kuwa ni ya mashambulizi makubwa tangu Israel iishambulie Palestina takribani wiki tatu zilizopita.
Mwandishi wa BBC aliyepo Gaza anasema watu wa familia saba wameuawa katika mpaka baina ya Israel na Palestina uliozingirwa.Bara bara zinaonekana kuwa tupu na moshi mweusi unaonekana kutoka katika eneo la Gaza huku mitambo ya umeme ikiwa imezimwa baada ya matanki ya mafuta kupigwa.Wanajeshi 10 wa Israel wameuawa siku ya Jumatatu wakiwemo wapiganaji watano wa Hamas walioingia Israel kupitia mahandaki ya chini kwa chini.Israel inasema imegundua mahandaki ishirini na mbili ya chini kwa chini eneo la mpakani kuingia Israel yanayounganisha mtandao mpana wa mahandaki hayo.
Maafisa wa afya katika utawala wa palestina wanasema kuwa watu 60 wameuawa. Israeli inasema imeshambuliwa maeneo sitini yakiwemo makao yasiyo na mtu ya kiongozi wa kundi la Hamas Ismael Haniya na vituo vya radio na runinga vya kundi la Hamas.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake ni lazima ijiandae kwa operesheni ya muda mrefu katika ukanda wa Gaza .
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa amesikitishwa na ripoti kuwa Israel ilisambaza ujumbe wa kuwaonya na kuwataka wenyeji kuondoka maeneo ya kaskazini mwa Gaza .
Ban amesema kuwa umoja wa mataifa hauna uwezo wa kuwakidhi watu zaidi wanaohama.