Maiti za watu waliouliwa na al-Shabaab Jumamosi asubuhi nje ya mji wa Mandera, Kenya, karibu na mpaka wa Somalia, zilipelekwa na wanajeshi hadi mjini humo.

Serikali ilikuwa inajitayarisha kusafirisha miili hiyo hadi mji mkuu, Nairobi.
Basi lililokuwa limebeba abiria 60 lilitekwa nyara alfajiri na abiria 28 walipigwa risasi na kuuwawa.
Wengi waliouwawa ni kutoka maeneo mengine ya Kenya ambao wakifanya kazi Mandera.
Inasemekana kuwa wengi wao walikuwa waalimu na wafanyakazi wa wizara ya afya ambao walikuwa wanarudi nyumbani kuwa na familia zao wakati wa Noeli.

Msemaji wa wapiganaji wa Somalia, al-Shabaab, alidai kuwa walihusika na shambulio hilo.
Wanajeshi na polisi wametumwa huko kwenda kuwasaka wale waliohusika na shambulio hilo lakini hakuna taarifa kuwa wamekamatwa.