Chande Abdallah/Mchanganyiko
MSANII wa muziki kutoka TMK Family, Chege Chigunda amezua gumzo la aina yake baada ya picha akiwa amevaa kitambaa cheusi kwenye mkono wake wakati akipafomu jukwaani kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akidaiwa kuwa ni hirizi.

Wasanii wa muziki kutoka TMK Family, Chege Chigunda wakishambulia jukwaa.
Picha hizo zilipigwa kwenye Tamasha la PSPF mkoani Dodoma lililofanyika February 20 Mwaka huu ambapo Chege na Temba waliokuwa wakipafomu jukwaani zilimuonesha Chege akiwa na fulana iliyokatwa mikononi yenye maandishi mekundu na meusi huku mkono wake wa kushoto ukiwa na kitambaa hicho.

Picha hiyo iliyotupiwa kwenye mitandao iliwashangaza watu waliodai kuwa ni mambo ya kiswahili huku wakikitaja kitambaa hicho kama hirizi, lakini wengine walidai kuwa kuna maelezo ya ziada kutoka kwa msanii huyo kwa kuwa kama angevaa hirizi asingevaa fulana aliyoikata mikono.
Mwandishi wetu alizungumza na Chege ambaye alikanusha taarifa za kuvaa hirizi na kudai kuwa hicho ni kitambaa cheusi ambacho wasanii wote waliokuwepo Dodoma siku hiyo walishauriana kukivaa wakiwa na maana ya kuguswa na msiba wa mwanamuziki mwenzao Mez B aliyefariki mapema siku hiyo.
“ Halafu nyinyi mwandishi (tusi) sana huwezi kusema mimi nimevaa hirizi wakati nilivaa kitambaa cheusi, wa hujui kuwa siku ile Mez B alikuwa amefariki. Acheni u(tusi) wenu,” aliongea kwa lugha chafu na kuongeza; “Subirini niongee na Shigongo sasa hivi,” alisema na kukata simu huku Temba, ambaye alikuwa naye pichani, akiwa hana kitambaa hicho.