AKutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi, Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislam Tanzania, Sheikh Ally Said Bassaleh, Mwenyekiti wa Wanawazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Suleiman Amran Kilemile na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Mohamed Issa.
BWanahabari wakifuatilia mkutano huo.
C.Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi, Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislam Tanzania, Sheikh Ally Said Bassaleh akizungumza jambo.
DViongozi hao wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).
KUELEKA Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu hapa nchini, Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay-Atul Ulamaa), wamewataka Watanzania kuilinda amani tuliyonayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, naibu katibu mkuu wa umoja huo, Mohamed Issa, amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu, viongozi wa dini zote hapa nchini wanatakiwa kuiombea nchi kuwa na amani huku wakiepuka kuziweka wazi hisia zao za chama.
Amesema kuwa, wao watahakikikisha amani iliyopo hapa nchini haitoweki hivyo wanawaomba wananchi kuungana nao kuilinda.
Aliongeza kuwa, wananchi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi hawapaswi kuwa na hofu kutoka kwa baadhi ya wagombea kwa kutoridhika na matokeo ya chaguzi kwenye kura za maoni.
Aidha aliwaomba Watanzania kujifunza kutoka kwa baadhi ya nchi zilizowahi kukumbwa na machafuko kama vile Burundi, Siera Lione, Kenya na DR Congo, ambazo ziliharibu sura ya nchi zao.