IRais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Orodha ya mawaziri katika serikali ya rais Muhammadu Buhari iliyosubiriwa kwa hamu sasa imetangazwa na spika wa bunge la seneti la Nigeria.
Buhari aliyechukua mamlaka miezi minne iliyopita alipata ukosoaji mkubwa kutoka kwa wapinzani wake na hata wajumbe wa chama chake kwa kuchelewa kuteua baraza la mawaziri.

Rais huyo amesema kuwa alichelewesha uteuzi huo ili kuwapata mawaziri ambao si mafisadi.
Na bila shaka raia wa Nigeria wamepumua sasa lakini baadhi yao wanasema kuwa majina mengine yaliyotokezea kwenye orodha hiyo yamewakatisha tamaa.
Orodha hiyo ina baadhi ya wanasiasa wakongwe, kukiwemo waliokuwa mawaziri na magavana.
Baadhi ya majina ya magavana wa zamani yamewatia hofu wananchi.
Kuna wale wanaosema kuwa kuchelewesha kutangaza majina ya mawaziri kumetoa mafanikio lakini wamesema kuwa hawaoni cho chote cha ajabu kwenye orodha hiyo.
Baadhi ya walioteuliwa ni watu wanaodaiwa kuwa wafisadi na kuna wale wanaodhani majina yao hayangeteuliwa.
Hata hivyo kuna wale wanaosema kwamba kwa kuwa wateule hao walifanya vitu vya manufaa katika maeneo yao ya kazi upungufu wao unapaswa kusahauliwa.
Wanaounga mkono orodha hiyo wanasema watu hao wataleta mafanikio waliyokuwa nayo katika majimbo yao kwa jukwaa la kitaifa.
Tangu uteuzi huo rais Buhari amesema kuwa yeye mwenyewe atasimamia wizara iliyo na utajiri mkubwa ya mafuta, ambayo wengi wanasema imejaa wafisadi.
Rais, hata hivyo alisema kuwa atamteua mdogo wake katika wizara hiyo ya mafuta atakayesimamia shughuli za kila siku katika sekta hiyo.
Baada ya kutangazwa kwa afisa mkuu wa kampuni ya kitaifa ya mafuta kama naibu ya waziri, tayari kuna uvumi unaoendelea kuwa atasimamia vyeo hivyo vyote viwili kwa mapenzi yake rais.
Rais Buhari alishinda uchaguzi kufuatia kampeni yake kuwa atakabiliana na ufisadi na uteuzi wa baraza lake la mawaziri unachunguzwa na wengi wanaotaka kuona kama hatua aliyochukua inalingana na ahadi zake.
Hii hapa orodha ya walioteuliwa:
Suleiman Adamu
Kemi Adeosun
Aisha Alhassan
Rotimi Amaechi
Solomon Dalong
Abdulrahman Dambazzau
Osagie Ehanire
Babatunde Fashola
Kayode Fayemi
Ahmed Musa Ibeto
Amina IbrahimI
brahim Usman Jubril
Emmanuel Ibe Kachikwu
Abubakar Malami
Lai Mohammed
Chris Ngige
Audu Ogbeh
Ogbonnaya Onu
Adebayo Shittu
Hadi Sirika
Udo Udom