Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel amesema hali ya tahadhari itaendelea kubaki kwa kiwango cha juu katika mji wa Brussels.
Waziri huyo amesema wasiwasi wa tishio la ushambulizi kama lililowahi kutokea siku kumi zilizopita mjini Paris bado ni mkubwa.
Lakini kuanzia Jumatano shule zitafunguliwa na usafiri wa treni katika mji mkuu utakuwepo tena.
Mamlaka ya Ubelgiji imesema mpaka sasa inawashtaki watuhumiwa wanne kwa kujihusisha katika shughuli zinazohusiana na ugaidi.