Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewasilisha ombi la kusamehewa kwa Rais wa nchi hiyo Isaac Herzog.

Ofisi ya rais ilisema Herzog atapokea maoni kutoka kwa maafisa wa haki kabla ya kulizingatia "ombi hilo lisilo la kawaida ambalo lina athari kubwa".

Netanyahu amekuwa akikabiliwa na keshi kwa miaka mitano iliyopita kwa tuhuma za hongo, ulaghai na uvunjaji wa uaminifu kuhusiana na kesi tatu tofauti. Hata hivyo, anakanusha kutenda kosa lolote.

Alisema katika ujumbe wa video kwamba angependelea kuona mchakato huo hadi mwisho, lakini masilahi ya kitaifa "yalidai vinginevyo".

Mapema mwezi huu, Rais wa Marekani Donald Trump alimtaka Herzog "kumsamehe kabisa" waziri mkuu