
KATIKA kuendeleza juhudi za Serikali kuboresha maisha ya Watanzania, Benki ya Azania imezindua huduma mbili za mikopo zinazolenga kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu pamoja na wafanyakazi katika sekta mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hizo “Boom Advance” na “Salary Advance”, Afisa Mwandamizi wa Idara ya Masoko wa benki hiyo, Elizabeth Nyattega, amesema kuwa hatua hiyo ni mwitikio wa mahitaji halisi ya wateja na ni ukombozi mkubwa kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi pamoja na wanafunzi. SOMA: MAJALIWA: Wizara ya Fedha Walindeni watumiaji wa huduma za fedha
“Benki ya Azania imeendelea kufanya maboresho makubwa katika utoaji wa huduma zake, hatua iliyotupatia tuzo ya Ubora wa Kidijitali Afrika Mashariki 2025 katika tuzo za Africa Bank 4.0 Awards 2025 zilizotolewa na taasisi ya kimataifa ya BII Finance mwaka huu,” alisema Nyattega.

Akifafanua zaidi, Nyattega amesema uzinduzi wa huduma hizo umezingatia mahitaji ya makundi yote nchini, hususan wanafunzi na wafanyakazi. “Kwa wanavyuo na watumishi wote nchini, hii ni fursa kubwa. Sisi kama benki tumehakikisha hakuna sababu ya mtu kukwama,” alisisitiza.
Kuhusu masharti ya mikopo, Nyattega amesema Boom Advance, ambayo inalenga wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, haitatozwa riba.Aidha, kwa upande wa Salary Advance kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa sekta binafsi, mkopo utatozwa riba nafuu ya asilimia 5 ya mshahara ili kumwezesha mfanyakazi kukidhi mahitaji yake ya kifedha kwa urahisi.
0 Comments