Kama angepatikana Don King wa ukweli Tanzania basi Jina la Mbwana Matumla lingekuwa mbali sana kwenye kona hii ya dunia.Mbwana Matumla ni kijana mdogo alipigana mapambano mengi sana na kujizolea sifa kemkem na kuipa umaarufu nchi yetu Tanzania.Kutokana na Mapromota bandia wanaojali maslahi yao wamewafanya mabondia wengi nchini kupoteza umaarufu wao kwa kuwapa mapambano ya mitaani na kuwashusha viwango vya juu walivyokuwa navyo.Hakuna hasiyejua jina Matumla katika fani ya ngumi,Ukoo huu umetuletea sifa sana Tanzania,sio tu ndani ya nchi bali hata nje ya nchi kwa ujumla.Ningeomba sasa serikali iangalie upya suala la kuwapa mapromota vibali vya kuwadhamini hawa mabondia wetu.Nikimuongelea Mbwana Matumla bado yungali fiti endapo atapatiwa Promota yoyote anaejali kwanza maslahi ya bondia.Angalia huyu Don King jinsi alivyokuwa akiwalipa mabondia na sasa walipo,Japo malalamiko ya hapa na pale hayakosi ila kuna unafuu kuliko mapromota wetu uchwara.Inakera sana na Inauma sana kuona mtu anadhulumiwa jasho lake.
0 Comments