Inasikitisha sana pale Serikali inapojitahidi kuleta vitendea kazi halafu sisi wananchi ndio wa kwanza kuviharibu.Tuliletewa kila aina ya vifaa kama muvionavyo pichani ila tu si kwamba vinafanana sawsawa na kwa matumizi mabaya tukaviharibu kwa muda mfupi tu.Yaliletwa magari mazuri ya kuzoa taka na badala yake tukawa tunaingiza vifaa ambavyo haturuhusiwi kuviingiza ndani ya magari yale na matokeo yake magari nayo yakaharibika kwa muda mfupi,Ndugu zangu ili nchi iendelee na kupendeza moja ya vigezo ni usafi,usafi ni afya kwani bila afya bora huwezi kufa nya kazi vizuri na hata mazingira yako unayoishi na kufanyika kazi pia yakiwa machafu ujue yanadidimiza akili kufikiri.Ona wenzetu jinsi wanavyopangilia usafi wao,kila dust bini unaweka unachoambiwa kuweka.Tuamke jamani sio kila kitu kuipa lawama Serikali.