Wadadisi wa mausala ya Kiuchumi wanahofia Sudan na nchi jirani zitapata hasara ya mabilioni ya dola ikiwa vita vita zuka upya.
Utafiti kuhusu athari za kiuchumi zitakazotokea ikiwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vitaibuka nchini Sudan unaonyesha kuwa taifa hilo na jirani zake litapata hasara ya $100 bilioni.
Ripoti iliochapishwa na baraza la ushauri wa maswala ya kiuchumi la Frontier Economics, inafichua kuwa iwapo kura ya maamuzi kuhusu uhuru wa Sudan Kusini itasababisha vita, huenda hasara ya asilimia thelathini na nne ya pato la kitaifa la Sudan katika kipindi cha miaka kumi ikashuhudiwa.
Wadidisi kutoka baraza hilo la kiuchumu, wameongeza kuwa uchumi wa nchi jirani kama vile Kenya na Ethiopia huenda ukapoteza dola bilioni moja kila mwaka baada ya vita kuanza.