Kampuni moja ya Ujerumani ya masuala ya Kompyuta SAP imeamrishwa kutowa takriban dola bilioni moja nukta tatu kwa kuiba siri za Kampuni nyingine.
Wanasheria wa kampuni hiyo ijulikanayo kama Oracle, wamesema kuwa adhabu hiyo ndiyo kubwa kuwahi kuwasilishwa katika kesi inayohusiana na utumiaji haramu wa hati miliki. Hicho ndiyo kiwango kilichoafikiwa na jopo la mahakama baada ya majuma matatu ya kusikiliza kesi hiyo.Halikadhalika uwamuzi huo umeonekana kuwa pigo kwa sifa na heshima ya mojawapo ya kampuni zinazotowa huduma katika biashara ya vifaa vya kopyuta duniani.
SAP daima imekiri kuwa mojawapo ya matawi yake iliyokuwa ikijulikana kama TomorrowNow -iliyotoweka ilinakili vifaa vya Oracle kupitia mtandao kwa ajili ya matumizi yake na kuwavuta wateja wa Oracle.
0 Comments