Imekuwa ni kitu cha kawaida kuona wanawake ni watu wa kuteswa na waume zao ila kwa wanaume kuteswa na wake zao ni kitu kama kinyume.Hali hii kwa dunia ya sasa tunaanza kuona ni kitu cha kawaida kwa mwanamke kumtesa mwanaume.Ila swali linakuja kwamba kwanini na sisi wanaume tunaoteswa na wake zetu hatusemi???Wao wanapoteswa tu mbio kuturipoti,kama si kwa wazazi wetu basi hata kwa wazazi wao watakwenda,ila kwanini na sisi wanaume tunaoteswa tunanyamaza kimya na tusiwaripoti mahala husika?