Baada ya timu ya Newcastle kuilazimisha sare ya goli 1-1 na timu ngumu ya Chelsea imekuwa sherehe kwa vinara wa Old Trafford Manchester United Kuin'gan'gania nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.Wakati huohuo timu ya Liverpool imepunguzwa makali yake kwa kubamizwa goli 2-1 na timu yenye makucha ya jogoo Tottenham Hotspurs na kuifanya Liverpool kuganda kwenye nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu.Kwa matokeo hayo ya jana timu ya MANCHESTER UNITED inaongoza ligi na kufuatiwa na CHELSEA FC wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na washika bunduki timu ya ARSENAL.