Baada ya kukutwa na hatia raia watano wa Kisomali wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.Ni wale waliofanya shambulizi katika utekaji wa meli za jeshi la kimarekani.
Hukumu hii ni ya kwanza nchini Marekani kuhusiana na kesi juu ya uharamia kwa karibu miaka 200. Watu hao wanakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha jela.Watano hao wamekutwa na hatia ya makosa ya uharamia, kushambulia meli, na kushambulia kwa kutumia silaha hatari.
0 Comments