Hatimaye washiriki watano wameingia fainali za shindano la Bongo Star Search na watachuana kumtafuta mshindi katika fainali itakayofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Washiriki hao wameingia katika hatua hiyo baada ya washiriki wenzao watatu kutangazwa kuaga shindano hilo jana wakati walipofanya ‘shoo’ kwenye ukumbi wa Water Front na kurushwa na kituo cha televisheni cha ITV.
kwa habari zaidi....Shoo hiyo ilipambwa na wasanii nyota kadhaa, wakiwemo Banana Zoro, Mwasiti, Tundaman, Maunda Zoro, Marlaw, Amani, Barnaba na Patricia Hilal, ambao waliimba pamoja na washiriki wa BSS.
Washiriki watano waliongia katika fainali hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi kutoka kwa wananchi ni Waziri Salum, Bella Kombo, Jemes Martin, Joseph Payne na Mariam Mohamed.
Washiriki watatu walioaga michuano baada ya kupata kura chache ni Christabella Nzowa, Haji Ramadhani na Chiby Dayo.
Mshindi wa BSS mwaka huu atajinyakulia zawadi ya Sh. milioni 30.
0 Comments