Kumekuwa na makabiliano makali katikati mwa jiji la London kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji wanaopinga ongezeko la karo ya vyuo vikuu nchini Uingereza.
Majengo ya serikali yalivamiwa na madirisha ya vioo kuvunjwa.Katika tukio moja, waandamanaji walivamia gari lililokuwa limembeba mrithi wa kiti cha ufalme nchini Uingereza mwanamfalme Prince Charles na mkewe Camilla.habari na picha zaidi gonga read more...
Walivunja kioo cha dirisha la gari hilo na kulimwagia rangi lakini wachumba hao hawakujeruhiwa.
Takriban watu hamsini wamejeruhiwa katika makabiliano hayo.Waziri mkuu David Cameron, ametaja machafuko hayo kuwa yasiyokubalika.
Katika tukio baya zaidi waandamanaji walikabiliana na polisi katika eneo la Parliament Square. Wengi walikamawa na kuzuiliwa kwa muda katika eneo la Westminster Bridge na maafisa wa polisi.
Polisi wamesema kuwa maafisa 12 na waandamanaji 43 wamejeruhiwa, huku watu 34 wakitiwa mbaroni.
Waziri mkuu David Cameron amesema ni ''jambo la kugutusha'' kwamba waandamanaji hao walivamia gari la mwanamfalme Charles.
Tukio hilo limejiri baada mpango wa serikali ya kuongeza karo ya vyuo kikuu mara tatu na kufikia dola alfu kumi na nne kwa mwaka kupitishwa na idadi ya kura ishirini na moja pekee.
Kwa kawaida miswada ya serikali ya mseto kati ya chama cha Conservative na Liberal Democrats bungeni huidhinishwa kwa zaidi ya kura themanini.
Hii ni kwa sababu wabunge wa chama cha Liberal Democrats waliamua kuheshimu mkataba ambao chama chao kilitia saini na kutoa ahadi ya kutoongeza karo ya vyuo vikuu wakati wa kampeni za uchaguzi.
0 Comments