Serikali ya Marekani ilifahamu kuhusu biashara ya silaha baina ya Kenya na Sudan ya kusini kwa mda wa miaka mingi, hayo ni kwa mujibu wa taarifa za hivi punde zilizovuja kupitia Wikileaks.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Wanabalozi wa Marekani chini ya Rais Barack Obama waliitaka Kenya isimamishe biashara hiyo mnamo mwaka 2009.habari zaidi gonga chini....Wakuu wa Kenya hawakufurahia hatua hiyo kwa sababu serikali ya awali chini ya Rais George W.Bush haikupinga msimamo wa Kenya katika kuisaidia Sudan ya kusini.
Mtandao wa Wikileaks kufikia leo umeisha chapisha kurasa zaidi ya 1,100 kati ya nyaraka 251,000 za siri za mawasiliano ya siri ya wanabalozi wa Marekani.
Nyaraka nyingi kutoka Ubalozi wa Kenya mjini Nairobi zinaelezea mazungumzo kuhusu safari ya Meli iliyokuwa ikielekea Kenya aina Faina iliyotekwa na maharamia wa Kisomali katika Ghuba ya Aden mnamo mwezi September mwaka 2008.
Meli hiyo ya Ukrainian iliachiliwa miezi mitano baada ya kikombozi cha dola milioni 3.2 ilikuwa na mzigo wa silaha, mkiwemo pia vifaru 30 vya kijeshi.
Serikali ya Kenya ilikanusha madai kuwa mzigo uliokuwa juu ya Meli Faina ulikuwa ni silaha za jeshi la Sudan ya kusini, SPLA.
Hata hivyo, nyaraka zilizochapishwa na gazeti la New York Times zimeonyesha kuwa wakuu wa Marekani walifahamu kuwa silaha zilizokuwa kwenye Meli ya Faina zilikuwa zikielekea Sudan ya kusini na walifahamu uhusiano wa Kenya katika Sudan ya kusini.
Licha ya utawala wa Rais Bush kutoingilia kati,serikali ya Rais Obama ilichukuwa msimami mkali na kuitisha Kenya kwa kuichukulia hatua ya vikwazo vikali.
Vifaru vilivyosafirishwa na Meli Faina inaeleweka kuwa bado viko nchini Kenya.
Gazeti la New York Times limearifu kuwa halina uhakika kama Marekani iliiomba Kenya ishikilie vifaru hivyo vilivyokuwa njiani kupelekwa Sudan ya kusini.
0 Comments