Katika mazingira magumu na ya kiistoria nchini Ivory Coast kumezuka mambo mengine tofauti kabisa katika nyanja ya siasa.
Ivory Coast iko katika janga kubwa la kisiasa, baada wa wagombea wote wawili wa urais kujiapisha kuongoza nchi.
Rais anayetetea kiti chake Laurent Gbagbo amekula kiapo cha kuongoza muhula mpya, lakini saa kadhaa baadaye Alassane Ouattara pia akala kiapo.Marekani, Umoja wa Mataifa na Ufaransa zimesema Bw Ouattara ndiye ameshinda uchaguzi huo.
Bw Ouattara alitanagzwa mshindi la Tume ya Uchaguzi, lakini matokeo hayo yalitenguliwa na Baraza la Katiba, ambalo linaongozwa na mshirika wa Bw Gbagbo.
Uchaguzi wa raindi ya pili ya urais, ulikuwa na lengo la kuliunganisha taifa hilo ambalo ndio mzalishaji mkubwa zaidi ya kakao duniani, baada ua kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002.
0 Comments