Swali-Ni wangapi huwa wanawasalimia wake zao kwa njia ya kuwapa mikono kama umuonavyo Mh: Jakaya Kikwete?Hii si mara yangu ya kwanza kumuona Mzee Kikwete akimsalimia hivi mkewe mara kwa mara huwa hajiangushi kumpa mkewe heshima inayostahili.Na hii ndivyo inatupasa wanaume tuliona adabu kwa wake zetu,na hii inatupasa kuwaheshimu na kuwapa haki stahiki wanawake,na hii ni mfano wa kuiga kwa wanaume wasio na tabia ya ustaarabu kwa wake zao.Maganga One Blog inampongeza sana Mh JK kwa hili kwani anaonyesha ni heshima gani na mapenzi gani kwa mkewe aliyonayo.Mungu awajaalie ndoa yenu idumu mpaka mwisho wa maisha yenu Amini.