Bwana harusi kulia ni ndugu Seif akiwa na bestman wake dakika chache baada ya ndoa.Ndoa hii ilifungwa usiku na kuhudhuriwa na wengi toka sehemu mbalimbali duniani.
 Mzee mtanashati mwenye koti la rangi ya dhahabu na saa ya Rado mkononi(Mzee Said Sleyum) ndiye baba wa bwana harusi,ni mzee maarufu jijini Dar es Salaam pande za Ilala,hakubaki nyuma pale alipopanda pipa kuja kumuozesha kijana wake jijini London.
Idara zote zilikamilika,watu walikula vyakula aina zote na kila mmoja alisifia jinsi chakula kilivyokuwa kitamu.Harusi hii hapakukosekana kitu,kwa waliohudhuria walisimuliana,Hongera bwana Seif tunakuombea kwa MUNGU ndoa yenu idumu milele na mpate watoto wema wenye maadili mema ya dini kama babu yao mzee Said.
Viongozi wa dini walitoa mawaidha ya kusisitiza jinsi ya kuishi na mke,na vilevile walishauri vijana kuepukana na maovu ya kidunia hivi sasa.Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislamu toka Oman,Pakistan,Saudi Arabia na hata Tanzania walihudhuria harusi hii ya bwana Seif iliyofanyika na kufana sana jijini London nchini Uingereza.Watu watajiuliza bi harusi mbona hatumuoni?Jibu ni kwamba yule ni mke wa Seif nasi hatupaswi kumuona bila ruksa maalumu toka kwa mumewe,na hizi ni taratibu nzuri ambazo zinapaswa kuigwa.

MAGANGA ONE BLOG INAMPONGEZA SANA BWANA SEIF,NA TUNASISITIZA KUOA MAPEMA NI VIZURI KWA VIJANA WA SASA KULIKO KUFANYA VITENDO AMBAVYO HAVIMFURAHISHI MUNGU...Hongera tena na tena bwana seif kwani harusi yako mlipendeza sana.