Sisi kila kitu ni mazabe tu,Jionee huyu jamaa pichani yupo bize kutengeneza Antena ya Tv ili akauze uswahilini kwa bei poa.Wanunuzi hawajui nini hatari ya kununua Antena zisizokuwa na ubora na viwango vilivyothibitishwa wao ni kujinunulia tu ili mradi maisha yaende,Ukiangalia amenunua tv ya laki mbili na nusu anakwenda kufungiwa antena ya shilingi elfu tano,kisha ikinyesha mvua na radi tv yake inaungua bila kujua nini chanzo cha tv yake kuungua.Tuwe makini twaweza kupoteza maisha kizembekizembe kwa uzembe na ujinga wetu.
0 Comments