Imekuwa kama itikadi kwa watoto wetu kuwapa majina ya baba zetu,mama zetu na hata ndugu zetu au marafiki zetu wa karibu inategemea tu wazazi mmejiandaaje.Uchunguzi nilioufanya ambao hauna uhakika watu wengi wamekuwa wakitoa majina ya watoto wao kwa shinikizo la wazazi wao(babu/bibi wa mjukuu huyo)kitu ambacho kimepitwa na wakati,Majina mengi yamekuwa ni kero kwa watoto hao wanapofikia umri fulani wa kuona haya.Kwahiyo sio vyema kutawaliwa na fikra za kizamani ambazo hazina misingi mizuri,Hakuna faraja yoyote ikiwa mtoto wako anakubugudhi kwa jina ulilomchagulia.Ushauri wangu sasa,wazazi kama wazazi tuna nafasi ya kuwachagulia watoto wetu majina mazuri ambayo hata wao wakiwa na wenzao mashuleni wanajisikia hasa kuwa hili jina nililopewa na wazazi wangu lilistahili kupewa mimi.Sina maana mbaya na wala nisieleweka vibaya,huu ni ushauri tu ni juu yako kusuka au kunyoa.Ahsanteni.
0 Comments