Pichani ni muhariri wa jarida la Summit Business nchini Uganda bwana Mustapha Mugisa ambaye amejikuta matatani baada ya jarida ulionalo pichani kuchapisha hiyo Katuni ya Raisi Yuweri Museven wa Uganda.Waandishi Habari wawili waliokuwa wamekamatwa nchini Uganda kutokana na kibonzo kilichochapishwa katika jarida lao wameachiliwa kwa dhamana, lakini wameamriwa kuripoti katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi, CID, ili kujieleza.
Walifika huko siku ya Alhamisi lakini wamesema hakuna walichoambiwa bali kuamriwa kurudi tena siku ya Ijumaa.
Mhariri wa jarida la kila mwezi Summit Business Review, Mustapha Mugisa pamoja na mchapishaji wake Dk Samuel Sejjaka, inadaiwa walikuwa na nia ya kumkejeli kiongozi wa taifa.
Walikamatwa mapema wiki hii, na wakili wao, Murungi Godwin, alisema wateja wake wamekuwa wakiripoti katika kituo cha polisi, pasipo kuchelewa, na kilichofanyika Alhamisi, ni kama kuwaongezea dhamana.
"Waliachiliwa kwa dhamana, na kutakikana kuripoti jana, na tulipofika hapo, afisa aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, alitueleza turipoti tena leo", alielezea Murungi.
Mhariri wa jarida hilo ambalo huchapishwa kwa Kiingereza, Mustapha Mugisa, alisema askari wapatao kumi waliingia afisini mwaka, na kumuuliza ikiwa yeye ndiye mhariri wa jarida hilo, na alipothibitisha hayo, walimuelezea lilikuwa na kibonzo, na ilielekea jarida lilikuwa na nia mbaya ya kisiasa, na hivyo wakamkamata.
0 Comments