Wafanyakazi watatu wa ndege wa Bulgaria wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa nchini Sudan wametekwa katika mji wa Darfur.
Kulingana na mpango wa chakula duniani wa umoja wa mataifa, WFP watatu hao, walitekwa na watu wenye silaha kwenye uwanja mdogo wa ndege.Bulgaria imethibitisha kwamba marubani watatu wametekwa Darfur.
Waasi katika mji huo wamekuwa wakipigana kwa muda mrefu na majeshi ya serikali na wapiganaji wa kiarabu.
WFP limesema watu hao watatu waliotekwa walikuwa wakilifanyia kazi shirika hilo.
Kulingana na taarifa ya majeshi ya kutunza amani ya umoja wa mataifa na umoja wa Afrika (Unmiss), watatu hao walitekwa siku ya Jumatano takriban kilomita 75 mashariki-magharibi mwa Geneina, mji mkuu wa jimbo la magharibi ya Darfur.
Wizara ya mambo ya nje ya Bulgaria ilisema watu hao waliotekwa walikuwa ni marubani wanaofanyia kazi kampuni binafsi
0 Comments