Mwanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wa Uganda(David Kato pichani) ambaye mwaka jana alilishtaki gazeti lililomtoa kwa jinsia yake hiyo amepigwa mpaka kufa.
Gazeti la Uganda la Rolling Stone lilichapisha picha za watu kadhaa ambao walisema ni wapenzi wa jinsia moja na huku pembeni kukiwa na kichwa cha habari "Wanyonge"
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria Uganda, na adhabu ya miaka 14 jela.
Mwandishi wa BBC Joshua Mmali, mjini Kampala, amesema haijakuwa wazi iwapo kifo hicho kina uhusiano na kampeni ya Rolling Stone lakini polisi wamesema hakuna uhusiano wowote baina ya harakati za Bw Kate na kifo chake.
Polisi wamesema licha ya kumkamata mshukiwa mmoja, mshukiwa mkuu- ambapo wanasema alikuwa akiishi naye amekimbia.
Hivi karibuni mbunge mmoja alijaribu kuongeza adhabu kwa kuwepo kwa hukumu ya kifo kwa baadhi ya makosa.
Kumekuwa na wimbi la matukio ya "mauaji kutumia chuma" huko Mukono, alipokuwa akiishi Bw Kato, ambapo watu wamekuwa wakiuliwa na vipande vya chuma.
Walioshuhudia wameiambia BBC kwamba mtu mmoja aliingia nyumbani kwa Bw Kato karibu na Kampala, na kumpiga mpaka kumwuua kabla hakuondoka.
Kundi lake liitwalo (Smug) limesema Bw Kato alikuwa akipata vitisho tangu jina, picha na anwani yake kuchapishwa na Rolling Stone mwaka jana.
Frank Mugisha, mkurugenzi mtendaji wa kundo hilo, aliiambia BBC kuwa "ameshtushwa" kupata habari hizo kutoka New York.
"Ameuliwa na mtu aliyeingia nyumbani kwake na nyundo, ikimaanisha mtu yeyote anaweza kulengwa."
Bw Mugisha alisema Bw Kato alikuwa na wasiwasi na vitisho alivyokuwa akivipata hivi karibuni.
Shirika la kutetea haki za binadamu (HRW) lilitoa wito wa kufanyiwa uchunguzi kwa kifo chake.
0 Comments