Enzi zangu mambo yalikuwa hivihivi,maana ukisema usubiri daladala utakesha,makondakta walikuwa hawana mchezo kabisaa wakisema achia gari ujue uachie gari vinginevyo utachafuliwa shati lako la shule!!na kuna wakati walikuwa wakitusukuma na kuhatarisha maisha yetu,kwa kweli Serikali inahitaji jitihada za makusudi ili kusaidia usafiri wa wanafunzi.Viongozi wengi wanajua juu ya hili ili wanajisahaulisha kama hawajui.Pichani wanafunzi wakiomba lifti eneo la Bunju nje ya jiji la Dar es Salaam.
0 Comments