Jamani ziara yangu ilikuwa hiviii....Shemeji yangu shoto kabisaa alinitembeza kwelikweli,alionesha kila kona ya jiji lao na haoo muwaonao hapo ni Mashosti zake full tabasamu,kwa kweli ilikuwa raha tupu kwa upande wangu.


Mwenyeji wangu ambaye ndiye mfadhili mkuu wa Blog hii alinitembeza madukani kuangalia hiki na kile,kwa kweli ilikuwa bomba kama vijana wa kileo wanavyoita,hapa ni katikati ya jiji lao nilipanda ngazi za umeme ambazo kwetu kulee Nzega zipo chache,nilifanya shopping ya macho tu (Window shopping ) kama alivyoimba 50 cent. 

Hapa ni chuo kikuu kimojawapo kilichopo pembezoni mwa mji wao,nilipata fulsa ya kwenda kuwaona baadhi ya Wanyamwezi wenzangu ambao wanapata mafunzo Hospitalini hapo,vilevile kama sunna nilipitia baadhi ya wagonjwa kuwapa pole hospitalini hapo.Kwa kweli nilizunguka vya kutosha japo sikutosheka na Ushamba wangu ( wa Nzega wa Nzega tu ).
Nipo supermarket zao hapooo!!,Full mazagazaga duuh mwanawane nilikuwa Flashizz sana tu.
 Wapenzi na wadau wangu wa Maganga One Blog,ziara yangu iliishia hapa,na hapo pichani ndio nilikuwa nimeshavuka utepe wa kuaga Mkoa wa Shemeji kuelekea kijijini kwanguuu Nzega.Kwa kweli ziara ilikuwa tamu tamu kupindukia.Nashukuru ndugu zangu kwa kila walilojaaliwa,kwangu ilikuwa faraja kubwa kwa likizo yangu na New Year Mungu awawezeshe Insh'Allah.Wapenzi wangu sasa nimerudi kijijini kazi kama kawaida yetu,tuendeleze mambo yetu.