Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, amekwenda Nigeria, kujadili msukosuko wa kisiasa wa Ivory Coast na Rais Goodluck Jonathan.
Bwana Odinga, ambaye ni mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika, atakutana na Marais wa Benin, Sierra Leone na Cape Verde siku ya Jumanne. Viongozi hao walikwenda Ivory Coast juma lilopita, lakini hawakuweza kumshawishi, Laurent Gbagbo aache Urais.Na Guillaume Soro, aliyeteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Alassane Ouattara, anayetambuliwa kimataifa kuwa Rais wa Ivory Coast, amesema Rais wa sasa, Laurent Gbagbo, anatumia njia za kuzinga mabadiliko ili apate kubaki madarakani.
Bwana Soro alisema lazima Bwana Gbagbo aondolewe.
0 Comments