Mama Rahma Al Kharous akiwa na viongozi wa timu ya Atletico Paranaense wakiwa wameshikilia bendera za mataifa mawili ikiwa ni ishara ya umoja katika michezo(Fair Play).Mama Rahma ndiye raisi wa Kampuni ya RBP Oil and Industrial Technology (T)Ltd.
Beki wa timu ya Paranaense ya Brazil Diego Alexandre Petri akikataa katakata kupitwa na kiungo wa timu kongwe ya Dar es Salaam Young Africa Abou Zubeir katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika katika uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Yanga ilikubali kwa shingo upande goli 3 - 2.
0 Comments